Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 13 wafa kwa baridi wakikimbilia Lebanon:UNHCR

Binti mkimbizi wa Syria akiwa bonde la Bekaa nje ya makazi wanayohifadhiwa wakati wa msimu huu wa theluji kali. Picha na :UNHCR/Andrew McConnell

Wakimbizi 13 wafa kwa baridi wakikimbilia Lebanon:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeelezea simanzi na masikitiko yake kufuatia vifo vya wakimbizi 13 wa Syria karibu na mpaka wa Masnaa Mashariki mwa Lebanon. Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi hao waliganda kwa theluji kali hadi kufa wakijaribu kuingia nchini Lebanon usiku kukiwa na baridi ya kupindukia kupiti njia ya usfirishaji haramu.

UNHCR inasema wakimbizi hao waliokuwa pamoja na wanawake, watoto na wanaume maiti zao zilikutwa Ijumaa na wengine Jumamosi. Hata hivyo kundi lingine la wakimbizi akiwemo mama mjamzito waliokolewa katika wakati muafaka na kukimbizwa hospitali kabla ya kuganda kwa baridi kali.

UNHCR inasema zahma hiyo ni Ishara ya hamasa ya wakimbizi hao wanaotaka kufika palipo na usalama nchini Lebanon na pia kuonyesha hali tete inayoendelea Syria. Wakati likituma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha shirika hilo limerejea wito wake kwa nchi zote duniani kuruhusu watu wanaohitaji ulinzi kuingia katika mipaka yao na kupata fursa ya kupita salama.