UNMISS yaimarisha doria ili kulinda raia Sudan Kusini
Kufuatia uamuzi wa raia wa Sudan Kusinikuanza kurejea nyumbani kutoka ukimbizini huko Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yao.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umeamua kuimarisha doria kwenye barabara ya Kaya hadi Yei ambayo hutumiwa na wakimbizi hao wanaorejea nyumbani.
Barabara hiyo kwa muda mrefu imetelekezwa na hivyo UNMISS kwa kushirikiana na mamlaka za jimbo la mto Yei.
Kamishna wa mji wa Morobo jimboni humo Richard Remo amesema ni muhimu kwa walinda amani hao kuwepo eneo la Kaya ili kuwapatia hamasa wakimbizi kurejea nyumbani kwa kuwa wataona wako salama.
Mamlaka za mji wa Morobo zimethibitisha kuwa tayari wakimbizi wameanza kurejea nyumbani na katika wiki tatu zilizopita wameshasajili wakimbizi wapatao 122 ambao wako katika hali mbaya wakisubiri misaada na maeneo bora ya kuwahifadhi.