Ethiopia yaawachia huru wafungwa wa kisiasa 115

19 Januari 2018

Osifi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imepongeza hatua ya serikali ya Ethiopia kuwaachia  huru wafungwa wakisiasa wapatao 115 waliokuwa  katika vifungo mbalimbali nchini humo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva hii leo ,Bi Liz Throssell ambaye ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Geneva amesema , hii ni hatua  nzuri iliochukuliwa na serikali ya Ethiopia   kuwaachia huru wafungwa hao ambao kwa nyakati tofauti walifungwa kwa vigezo vya kupaza sauti zao na kuonyesha msimamo tofauti na  uongozi ulioko madharakani, kitu ambacho ni haki ya msingi kwa wananchi. Na kuongeza

(Sauti ya Liz Throssel)

“Tunafahamu kwa kiwango gani baadhi ya wafungwa waliweza kuwa wamevunja sheria. Lakini tunahimiza Serikali kuhakikisha kuwa uvunjaji wa sherai uliofanywa unalingana na adhabu za wafungwa na kuepusha matukio yanayosababisha  baadhi ya wafungwa kuwekwa hatiani kinyume cha cheria. Pia tunakumbusha kuwa lazima mahakama ifanye kazi yake bila kuwepo na upendeleo wa kikabila ,wala walikotoka watu.”

Bi Liz amesema serikali ya Ethipia imeridhia kupitia upya sheria zake ili kutoa kipaumbele katika masuala ya ugaidi, haki za kibinadamu na usawa kwa wote.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter