Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watalii duniani ilipanda 2017 na huenda ikaongezeka zaidi :UNWTO

Wanyama wa piri katika eneo la utalii barani Africa. Picha: UM

Idadi ya watalii duniani ilipanda 2017 na huenda ikaongezeka zaidi :UNWTO

Idadi ya watalii wa kimataifa, wanaowasili katika nchi nyingine, na watu wanaoingia nchi moja kwa siku kwa njia  halali iliongezeka mwaka wa 2017 kwa kiwango cha asili mia 7 na na hivyo  kufikia watalii Zaidi ya millioni elfu moja na mia tatu.

Hii ni kwa mujibu wa vigezo vipya vya shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii duniani UNWTO. Shirika hilo linabashiri kuwa ongezeko hilo litazidi kuvuma mwaka 2018 kwa kiwango cha asili mia  kati ya nne na tano.

Kuongezeka kwa watalii duniani kunatokana na uwepo wa takwimu za kuwasili sehemu zote duniani, na kukisiwa kuwa kuwasili kwa  watalii  duniani kote mwaka 2017 kulipanda kwa asili mia saba ambayo ni mkubwa zaidi kutokea tangu mwaka 2010 na kuwasilisha matokeo makubwa kwa kipindi cha miaka saba. Hii inaonyesha kama mkondo waumiminikaji wa watalii ulipanda zaidi ya ule uliokuwepo kabla wa asili mia nne.

Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili, amesema kuwa usafiri wa kimataifa unaendelea kukua na hivyo kuimarisha sekta ya utalii kama msingi unaosukuma gurudumu la maendeleo.

Aidha amesema sekta hiyo inavyoendelea kukua ni sharti kushirikiana  kuhakikisha kuwa ukuaji huu unamfaa kila mwanachama wa jamii mwenyeji  na pia kwenda sanjari na malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s.