Skip to main content

Vikosi vya UNAMID vyaendelea kupunguzwa Darfur: Ngondi

Walinda amani wa UM wapiga doria Darfur Sudan. Picha: UNAMID

Vikosi vya UNAMID vyaendelea kupunguzwa Darfur: Ngondi

Vikosi vya kulinda amani vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur nchini Sudan UNAMID vinaendelea kupunguza askari wake wasikohitajika na kuelekeza nguvu zake katika maeneo ambayo hayajapata huduma kwa muda mrefu, amesema leo mkuu wa vikosi hivyo. John Kibego anatupa taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Luteni Jenerali Leonard Ngondi ameyasema hayo akihitimisha ziara yake katika eneo la Minawashe kuliko na kambi zinazokaliwa na walinda amani wa UNAMID kutoka Tanzania.

Ameongeza kuwa kufuatia zoezi hilo la kupunguza vikosi sasa kazi za ulinzi wa amani zitahamia eneo la Jaber Mara Mashariki ambako kimeundwa kikosi kazi kitakachohusisha kambi 10 zinazozunguka eneo hilo ikiwemo kambi zinazokaliwa na askari wa Tanzania huku kambi za maeneo mengine zikifungwa. Amesema hata hivyo matarajio ni makubwa

(SAUTI YA LT JENERALI NGONDI )

Luteni Jenerali Ngondi mezitaja kambi hizo kuwa ni Minawashe, Khor Abeche na Shangilitobaya, Kass, Tawila, Kapya, Sontoni, Golo, Netiti na Jalinje ambayo ndio itakuwa makao makuu ya kikosi kazi hicho.

Amesisitiza kuwa lengo kuu la kujikita katika eneo hilo ni kuhakikisha huduma ya UNAMID inawafikia wakazi wa Jaber Mara ambao kwa muda mrefu hawakuweza kupata huduma kutokana na usalama mdogo na miundombinu duni.