Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

61 wafa, na mamia waambukizwa Listeria Afrika Kusini: WHO

Nyama ya ng'ombe. (Picha:UN /JC McIlwaine)

61 wafa, na mamia waambukizwa Listeria Afrika Kusini: WHO

Watu 61 wamefariki dunia na wengine kwa mamia wameambukizwa katika mlipuko wa ugonjwa wa Listeriosis nchii Afrika Kusini limesema leo shirika la afya duniani WHO. Selina Jerobon anaarifu Zaidi

(TAARIFA YA SELINA)

Kwa mujibu wa WHO mbali ya vifo jumla ya visa 748 vimethibitishwa maabara hadi sasa ni  ugonjwa ambao unaosababishwa na vijidudu aina ya bakteria vinavyopatika kwenye vyakula vitokanavyo na mifugo, matunda na mbogamboga.

Bakteria hao humuathiri binadamu kwa kula vyakula hivyo vikiliwa vibichi, havikuchemka au havikuiva vizuri kama vile maziwa,nyama, matunda na mboga za majani.

Dalili za Listeria ni pamoja na kuhara, kutapika nahoma.Kupitia msemaji wa WHO Chriastian Lindmeier mlipuko huu wa listeria Afrika Kusini ni mkubwa kabisa kuwahi kutokea duniani na kwamba wadudu hao wa bakteria

(LINDMEIER CUT 1)

“Wanaweza kumuathiri mtu yeyote , lakini Zaidi wale walio na kinga hafifu mwilini hivyo watoto mara nyingi ndio waathirika wakubwa na watoto wachanga ni karibu asilimia  40 ya waathirika wote.”

Ameongeza kuwa ugonjwa huo unachukua muda mrefu kubainika na hivyo

(LINDMEIER CUT 2)

“Hii ni changamoto kubwa tunayokabiliana nayo, ni muhimu kupika  vizuri nyama, chakula chako, uwe makini na maziwa yasiyochemshwa na hususani kwa watu wenye kinga hafifu au kina mama wajawazito, wazee, watu wanaoishi na HIV na watu wenye saratani wako katika hatari atari wawe makini na jinsi wanavyoandaa chakula chao na nini wanakula.”

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Johanesberg, Gaoteng na Pretoria. Nchi zingine ambazo zimewahi kupata mlipuko huo ni pamoja na Marekani 2011 na Italia 1997.