Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saidieni watoto mtaani Mogadishu: UNICEF /Save the children

Watoto katika kambi isiyo halali ya wakimbizi wa ndani iliyolazimika kufungwa Somalia. Picha: UNICEF/Video capture

Saidieni watoto mtaani Mogadishu: UNICEF /Save the children

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake wameisihi jamii ya kimatataifa kusaidia watoto walio kwenye mazingira magumu baada ya kukosa makazi huko Mogadishu nchini Somalia. Joseph Msami na ripoti zaidi.

(Taarifa ya Joseph Msami)

Wito huo unafuatia bomoabomoa ya mwezi uliopita ya makazi ya zamani ya serikali kupisha ujenzi wa mji na kusababisha  zaidi ya familia 4000  za wakimbizi wa ndani waliokuwa wanaishi katika majengo hayo yaliopo katika  kata ya Kahda huko Mogadishu.

Hivi sasa familia hizo hazina pahala pa kuishi.

UNICEF na wadau wake Save the Children wamesema waathirika wakubwa katika sakata hilo ni wanawake na watoto amabao walitolewa kwenye makazi hayo bila taarifa  hivyo kupoteza mali zao.

Tayari mashirika hayo yametoa misaada ya dharura kama vile maji, vifaa vya shule kwa wanafunzi na pia imesaidia kuunganisha  familia 35 zilizokua zimetengana wakati wa zoezi  la bomoabmoa.

Halikadhalika wametoa msaada wa blanketi, mahema, sabuni na magodoro.

UNICEF na Save the children wametoa wito kwa serikali ya Somalia kuhakikisha usalama wa watoto pamoja na familia zao katika kipindi hiki ambapo wapo mtaani bila msaada