Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leila Zerrougui kuongoza MONUSCO

Bi. Leila Zerrougui kutoka Algeria ameteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC, MONUSCO . (Picha:MONUSCO)

Leila Zerrougui kuongoza MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC, MONUSCO umepata kiongozi mpya naye si mwingine bali Bi. Leila Zerrougui kutoka Algeria.

Hatua hii inafuatia uteuzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambapo Bi. Zerrougui atakuwa Mwakilishi wake maalum nchini DRC.

Bi. Zerrougui ana uzoefu wa miaka 30 katika masuala ya sheria na ulinzi na pia  ni mtaalamu wa masuala ya utawala, na aliwahi kushika wadhifa wa juu kama naibu muakilishi wa MUNUSCO kati ya 2008 hadi 2012 katika ulinzi wa raia katika ukanda huo.

Akiwa mtaalamu na mtetezi wa masuala ya haki za bindamu katika Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa,  Bi Zerrougui amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za waathirika wa unyanyasaji ambao wengi wao ni wanawake na wasichana katika migogoro mbalimbali ya kivita duniani.

Kufuatia uteuzi huu, Bi Zerrougui anamrithi aliyekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko DRC  Maman Sambo Sikidou.