Utalii ifikapo 2030: Neema au janga?

27 Disemba 2017

Watalii wapatao bilioni 1.8 wanatarajiwa kuwa wametembelea nchi mbalimbali kwa ajili ya utalii ifikapo mwaka 2030, limesema shirika la utalii la Umoja wa Mataifa, UNWTO likionya kuwa mwenendo huo unaweza kuwa fursa au janga duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa UNWTO Taleb Rifai ameiambia Idhaa ya Umoja  wa Mataifa kuwa mwelekeo huo unaweza kuwa fursa au janga kwa kutegemea vile ambavyo kila nchi itaweka sera kwa kuzingatia ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kwa kuwa...

(Sauti ya Taleb Rifai)

“Watalii bilioni 1.8 wanaweza kuleta fursa bilioni 1.8 au majanga bilioni 1,8. Inategemea unafanya nini. Majanga kama vile utumikishaji watoto, biashara ya ngono na usafirishaji haramu wa rasilimali za kitamaduni, ambavyo vyote hufanyika kupitia miundombinu ya kitalii.”

Hata hivyo amesema kuna fursa akitolea mfano huko Mexico ambako kwenye kitongoji cha Riviera de Maya karibu na mji wa Cancun..

(Sauti ya Taleb Rifai)

“Rasilimali zilizopo zimetumika kurejesha mikoko iliyoharibiwa na binadamu. Na kwa kufanya hivyo inakuwa kivutio na hivyo uhifadhi wa maliasili hizi zinakuwa ni rasilimali adhimu kivutio kwa wasafiri na watalii.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter