Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka kujifungulia watoto kwenye lori hadi kupata kituo cha afya

Francesca alipambana hadi Benki ya Dunia ikasaidia kuwajengea kituo cha afya kijijini kwao huko Papua New Guinea. (Picha:video-Benki ya Dunia)

Kutoka kujifungulia watoto kwenye lori hadi kupata kituo cha afya

Nchini Papua New Guinea, wanawake wamechukua hatua kulinda afya zao. Baada ya safari za kutwa kucha kufuata vituo vya afya vilivyokuwa vinapatikana umbali mrefu, wanawake walishikamana na kusaka usaidizi kutoka Benki ya Dunia ili kuanzisha kituo cha afya kwenye kijiji chao. Hatua hii inaenda sambamba na lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG linalotaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa kila mtu ana afya nje na ustawi wake unalindwa. Sasa huko Papua New Guinea,  hali ilikuwa mbaya hadi wajawazito wanajifungulia watoto kwenye lori. Lakini sasa nuru siyo tu imebisha hodi bali imeingia. Je wamefanya nini? Flora Nducha ndio mwenyeji wako.