Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki waeneza amani Somalia

Nchini Somalia kila mbinu yatumika ili kuchagiza na kuendeleza amani. (Picha:UNSOM Video)

Muziki waeneza amani Somalia

Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, Somalia imeghubikwa na migogoro ikiwemo mashambulizi ya Al-Shabaab na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kusababisha maelfu ya raia  kupoteza maisha, makazi na wengine kusaka hifadhi nchi jirani. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini humo, UNSOM, kwa kushirikiana na serikali unatumia njia mbalimabli kuhakikisha mkataba wa amani umetekelezwa ili  watu waweze kurejea makwao. Je ni mbinu gani zinatumika kuchagiza amani? Joshua Mmali anaangazia kupitia makala hii.