Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid haachii ngazi wala hajiuzulu:UN

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’aad al-Hussein. Picha: UN/Jean-Marc Ferré

Zeid haachii ngazi wala hajiuzulu:UN

Ofisi ya Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Geneva, leo imetoa ufafanuzi kuhusu Kamisha mkuu Zeid Ra’ad al Hussein kutosaka muhula wa pili madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari ili kutoa ufafanuzi wa kwanini Zeid ameamua kuishia na muhula mmoja wa miaka minne tu ,msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville amesema wakati sifa na pongezi kemkem zikiendelea kumiminika kwa Kamisha huyo kwa kazi nzuri na jinsi anavyosimama kidete kupigania haki za binadamu bila woga, pia wana wasiwasi kwamba uamuzi wake umetafsiriwa vinginevyo.

Amesema kichwa cha habari kwenye moja ya taarifa zilizochapishwakuhusu suala hilo kimesema “2017 ni mwaka ambao hata Kamishina mkuu wa haki zabinadamu wa Umoja wa Mataifa amekata tamaa kuhusu haki hizo” amesema kichwa hicho kinapotosha na si kweli kwani,

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

“Kinyume na ripoti nyingi hukusu suala hilo, haachii ngazi wala hatojiuzulu, ni kinyume kabisa. Ana mkataba wa miaka minne na atautumikia kipindi chote bila woga wala upendeleo, mpaka siku ya mwisho ambayo ni tarehe 31 Agosti, zaidi ya miezi minane ijayo.”

Ameongeza kuwa hakuna kipya kwa Kamishina kuhudumu kwa muhula mmoja tu wa miaka minne, na ukweli ni kwamba ni kamishina mmoja tu kati ya sita waliowahi kuongoza ofisi hiyo ndiye aliyehudumua mihula miwli ambaye ni Navi Pillay , hivyo muhula mmoja ni kawaida cha ajabu ni zaidi ya muhula mmoja.