Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je wafahamu maana ya neno mzimu?

Je wafahamu maana ya neno mzimu?

Wiki hii tunaangazia neno "Mzimu" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno “Mzimu” lina maana zaidi ya moja. Maana ya kwanza ni mahali pa kufanyika matambiko ambayo ni chini ya miti mikubwa kama mbuyu au mkuyu au hata kwenye mapango. Maana ya pili ni kivuli cha sura ya mtu ambaye amefariki dunia. Maana ya tatu ni maskani ya watu waliofariki dunia kama vile makaburini ambako watu wanaweza kwenda kufanya mawasiliano na ndugu zao waliofariki dunia.