Mapigano ya kikabila DRC yapamba moto huku jeshi la DRC likifurushana na ADF

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda. (Picha:© UNHCR/Isaac Kasamani)

Mapigano ya kikabila DRC yapamba moto huku jeshi la DRC likifurushana na ADF

Watu zaidi ya 2600 wamefungasha virago kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na kuingia Uganda kusaka usalama huku maelfu wengine wakitarajiwa kufuatia mapigano ya kikabila yanayoshika kasi na sasa mashambulizi ya Uganda dhidi ya waasi wa ADF Kivu ya Kaskazini .

Kupata taarifa zaidi naungana kwa njia ya simu na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye hivi sasa yuko kambini Hoima ambako wakimbizi wengine wanahifadhiwa, Kibego nini kinachoendelea hivi sasa?

UNHCR inasema kuwa idadi k ubwa ya wakimbizi wanavuka ziwa Albert kwa kutumia mashua ndogo za uvuvi na kuwasili eneo la Sebagoro, kijiji kilichopo kilometa 270 Kaskazini-Magharibi mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.

UNHCR inaongeza kuwa wakimbizi hao wanakimbia wakiwa na virago muhimu ikiwemo mifugo na pikipiki.