Mpatanishi anapofungasha virago ni mashaka- Dkt. Salim

Dkt. Salim Ahmed Salim, mwanadiplomasia nguli kutoka Tanzania ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali kwenye Umoja wa Mataifa ikiwemo Rais wa mkutano wa 34 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1979. (Picha: UN/Maktaba)

Mpatanishi anapofungasha virago ni mashaka- Dkt. Salim

Hatma ya amani Mashariki ya Kati hususan kati ya wapalestina na waisraeli imeingia dosari baada ya Marekani kutangaza kutambua Yerusalem kama mji mkuu wa Israel. Marekani ikichukua msimamo huo nchi 128 wanachama wa  wa Umoja wa Mataifa wamepitisha azimio la kuitaka nchi hiyo ibadili uamuzi huo, uamuzi ambao unaenda mbali zaidi na kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka mji mkuu wa sasa wa Israel, Tel Aviv kwenda Jerusalem. Lakini nini maana ya hatua hizi? Flora Nducha amezungumza na Dkt. Salim Ahmed Salim mwanadiplomasia nguli kutoka Tanzania ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika OAU, sasa muugano wa Afrika.