Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICTY muasisi wa haki duniani- Guterres

Jengo la makao makuu ya mahakama ya kimataifa kwa uhalifu uliofanyika katika Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia, ICTY huko The Hague, Uholanzi. (Picha: ICTY)

ICTY muasisi wa haki duniani- Guterres

Hatimaye mahakama ya kimataifa iliyokuwa inaendesha kesi za uhalifu uliofanyika kwenye iliyokuwa Yugoslavia, imefunga pazia rasmi leo baada ya kuhudumi kwa miaka 24.

Hatimaye mahakama ya kimataifa iliyokuwa inaendesha kesi za uhalifu uliofanyika kwenye iliyokuwa Yugoslavia, imefunga pazia rasmi leo baada ya kuhudumi kwa miaka 24.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza huko The Hague, Uholanzi hii leo wakati wa hitimisho la ICTY, ameielezea kuwa ni muasisi wa haki ya kimataifa.

Katika kipindi cha uwepo wake, ICTY imehukumu watu 90 kwa uhalifu waliotenda huko Yugoslavia ikiwemo mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu wa kibinadamu wakati wa vita vya Balkan miaka ya 90.

Na kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesema..

(Sauti ya Guterres)

"Mahakama ya kimataifa kwa uhalifu uliofanyika kwenye iliyokuwa Yugoslavia imekuwa muasisi wa kuunda mfumo wa kisasa wa haki ya kimataifa dhidi ya uhalifu. Mahakama hii imevuka kile kilichotarajiwa wakati ikianzishwa mwaka 1993. ICTY imebadili jinsi ya kuzungumza na kushughulikia mazingira ambamo kwayo uhalifu wa kimataifa umefanyika.”