Takribani watu 500 wakimbia mzozo DRC: UNHCR

20 Disemba 2017

Nchini Uganda wakimbizi wanazidi kumiminika kila uchao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo habari zinasema kuwa kuanzia jana hadi leo takribani watu 500 wameingia nchini humo wakikimbia ghasia nchini DRC. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Kulingana na James Karanja, Mkuu wa Ofisi ya UNHCR ya Hoima, wakimbizi hao tayari wameasilishwa kwneye kambi ya Kyangwali iliopo kilomita tatu tu kutoka kwenye ufukwe wa Ziwa Albert, linalopakanisha Uganda na DRC.

(Sauti ya James Karanja)

Wamekuwa wakivuka Ziwa kweney mitumbwi hatari na kuwasili kwenye fukwe za Sebagoro na Bugoma wilayani Hoima.

(Sauti ya James Karanja)

Bwana Karanja amesema baado hawajafahamu sababu halisi yao kukumbia.

(sauti ya James Karanja)

Hata hiyvo, baadhi ya wakimbizi wanadai kukimbia mzozo wa kikabila unaohusisha jamii za Wahema, Wagegere na Walendu  wilayani Ituri.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter