Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchumia juani hulia kivulini- Magdalena

Mjane aliyepitia madhila mengi kufuatia kifo cha mumewe, Magdalena Mbiya Namutebi. Picha: John Kibego

Mchumia juani hulia kivulini- Magdalena

Mila za baadhi ya makabila katika bara la Afrika, zimesheheni changamoto za unyanyapaa kwa wajane wanapodai au kupigania mali za waume zao. Mara nyingi wanawake hao huishia kunyanganywa kila kitu na ndugu wa marehemu na kusababisha mgawanyiko katika familia.

Nchini Uganda , Bi Magdalena Mbiya Namutebi ni mmoja tu kati ya  mamilioni ya wanawake ambao walipoteza kila kitu baada ya kufiwa na mumewe. Kutokana na ujasiri wake Magadalena hakukata tamaa, peke yake aliwalea watoto wake wanane, akawasomesha mpaka alipofikia wakati ya kuvuna matunda ya kazi ngumu aliyoifanya. Je alifanya nini? ungana na mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda katika makala hii…