Hali bado tete kwa wanawake na watoto CAR- UNICEF

19 Disemba 2017

Mwaka 2017 umekuwa ni mwaka mgumu zaidi kwa maisha ya wanawake na watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR/

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, ikisema hakuna hata nuru kuwa hali itakuwa bora siku zijazo kutokana na hali ya usalama kuendelea kudorora.

Kwa mujbnu wa ripoti hiyo, vurugu na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe inazidi kuongezeka  katika mikoa ya kaskazini magharibi na kuathiri maisha ya watu wengi ikiwemo  wanawake na watoto hivyo  kusababisha ukimbizi wa ndani.

Chistina Muhigana ni mwakilishi wa UNICEF nchini CAR.

(Sauti ya Chistina Muhigana )

“Vikundi vilivyojihami mara kwa mara vinashambulia misafara yenye misaada ya kibinadamu. Mwaka huu pekee wafanyakazi 14 wa misaada ya kibinadamu wamepoteza maisha yao nchini CAR, na mashirika ya usaidizi yalichukua uamuzi wa kusimamisha shughuli zao kwa maeneo kadhaaWatoto na wanawake ni waathirika  wakubwa katika migogoro hii na karibu  nusu ya watu wa CAR ambao ni milioni 2,  wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na watoto milioni 1.3.”

Ingawa kuna changamoto ya kiusalama UNICEF inatoa wito kwa wahisani kuendelea kusadia jitihada zao katika kutoa huduma za kibinadamu CAR  ikiwemo elimu kwa watoto zaidi ya 50,000 na huduma za afya kwa  wanawake na wazee.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter