Wacameroon wanaoingia Nigeria wapata msaada:UNHCR

19 Disemba 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeongeza uwepo wake Kusini Mashariki mwa Nigeria ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu wanaokimbia machafuko katika eneo la Cameroon linalozungumza Kiingereza na kuingia Nigeria. Selina Jerobon na tarifa kamili.

(TAARIFA YA SELINA JEROBON)

Kwa mujibu wa Andrej Mahecic msemaji wa UNHCR Geneva, tangu kuchaha kwa mvutano baina ya vikosi vya usalama vya Cameroon na waandamanaji wanaounga mkono demokrasia katika jimbo linalozungumza Kiingereza mwezi Oktoba, kwa pamoja UNHCR na timu za serikali wameorodhesha waomba hifadhi 7,204 katika vijiji vya Nigeria kwenye jimbo la Cross River wakikimbia machafuko na wengine kwa maelfu bado wanasubiri kuandikishwa. Ameongeza kuwa“Asilimia 70 ya waomba hifadhi walioorodheshwa wanatoka katika eneo la Akwaya Kusini Magharibi mwa Cameroon . Wanawake na watoto ndio wengi, wanahifadhiwa na jamii za karibu na mpakani lakini wakati machafuko nchini Cameroon yakiendelea waomba hifadhi wengi zaidi wanaendelea kuwasili , na UNHCR inahofia kwamba uwezo wa jamii inayowahifadhi punde utazidiwa nguvu.”

Pia amesema fedha zaidi itakuwa ni lazima ili kuweza kuwasaidia wanaowasili, kuratibi na kuchukua hatua, ingawa kwa sasa UNHCR na washirika wake wameandaa mipango ya dharura.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter