Mbinu za kupunguza njaa zazaa matunda Nigeria
Hiki kitakuwa chakula chakunitosha mimi na familia yangu na kingine nitauza na pesa nitatumia kuwapeleka watoto shule.
Hii ni kauli ya leo Aisha Ibrahim ambayo haikuwahi kusikika kwa miaka 3 iliyopita lakini leo Aisha anaisema baada ya kuvuna mazao yake huko Yobe nchini Nigeria.

Baadhi ya mbegu yaliyosambazwa na FAO kusaidia wakulima wakimbizi. Picha: FAO
Yobe ni moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mashambulizi ya Boko Haramu lakini baada ya waasi hao kuondoka na wananchi kusaidiwa kurejea katika makazi yao na kupatiwa misaada mbalimbali maisha yameanza kurejea kawaida.

Ripoti zinaonesha kupungua kwa njaa Nigeria. Picha: FAO
Ripoti zinaonesha kupungua kwa njaa kwenye maeneo yaliyokuwa na vita ambapo sasa idadi ya watu wenye njaa imepungua kutoka watu Milioni 5.2 hadi milioni 2.6 kwa kipindi cha miezi mitatu pekee

Ripoti ya awali ya kiwango cha njaa Nigeria. Picha: FAO