Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Apu kwa ajili ya wahamiaji yazinduliwa:IOM

Picha: IOM
Apu mahsusi kwa ajili ya wahamiaji.

Apu kwa ajili ya wahamiaji yazinduliwa:IOM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limezindua Apu mahsusi kwa ajili ya wahamiaji ijulikanayo kama MigApp.

Apu hiyo ni nyenzo inayochukua fursa ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano iliyosambaa ya simu za viganjani ili kuwa na jukwaa moja la mawasiliano ambapo wahamiaji wanaweza kuwa na fursa ya kupata tarifa za wakati huu, za kuaminika, zinazoweza kuwasaidia na pia huduma za IOM.

Kwa mujibu wa IOM , Apu hiyo itawasaidia wahamiaji kufanya maamuzi kwa wakati wote wa mchakato wa uhamiaji wao, kwani uhamiaji wa kiholela na usio salama unafanyika kwa sababu ya watu kukosa uelewa wa hatari zilizopo katika mchakato huo, kupewa taarifa za uongo kuhusu masuala ya visa, hatari za kiafaya na sheria za safari, kuwa na huduma hafifu au kutopata kabisa huduma za msingi na kutokuwa na jukwaa linaloweza kuwapa taarifa za mara kwa mara za masuala ya uhamiaji na huduma.

Hivyo shirika hilo linatarajia kwamba Apu hiyo sasa itakuwa mkombozi na nyenzo muhimu kwa ajili ya kuwasaidia wahamiaji.