Uingereza yaitikia wito wa WFP

18 Disemba 2017

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limepokea dola milioni 67 kutoka Uingereza ili kusaidia  mahitaji ya kibinadamu nchini Yemen.

 
Nicolas Oberlin ambaye ni Naibu Mkurugezi wa WFP kanda ya Mashariki ya Kati amesema fedha hizo zitasaidia kuokoa maisha ya zaidi ya watu Laki sita na nusu ambao wanakabiliwa na tatizo la njaa.
 
Watu hao pia hutegemea misaada ya shirika hilo kama huduma za Afya, maji, chakula petroli na kadhalika.
 
Aidha Bwana Oberlin amesema Uingereza ni kati wa wahisani muhimu na  wanaotegemewa na shirika hilo kutokana na mchango wake katika kusaidia  zaidi ya watu milioni 8.4  nchini Yemen ambao ni waathirika wa vita na njaa.
 
Mchangao huu si wa kwanza wa Uingereza kwa WFP kwa ilishapatia shirika hilo zaidi dola  milioni 100 kwa shughuli za kibinadamu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter