Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko mapya, misaada ya kibinadamu zaidi yahitajika YEMEN

© UNHCR/Shabia Mantoo

Machafuko mapya, misaada ya kibinadamu zaidi yahitajika YEMEN

Machafuko mapya yameibuka magharibi mwa pwani ya Yemen na kusababisha watu kuyakimbia makazi yao

Zaidi ya watu 1,400 wamekimbilia majimbo ya Taizz na Hudaydah na kwenda maeneo mengine ambako huko wanahitaji misaada ya kibinadamu

Msemaji wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch amesema kuwa tayari misaada ya dharura imepelekwa kwa zaidi ya familia 2000 huko Hudaydah.

Hata hivyo kwa kuwa bandari ya Hudaydah imefungwa, wameshindwa kuwasilisha vifaa kama vile vile banketi,  vyakula na dawa vilivyomo kwenye kontena 43 bandarini humo.

UNHCR imeziomba mamlaka za Yemen kuharakisha utoaji wa mizigo hiyo kwa kuwa inahitajika sana na kuna bidhaa zinazoharibika mapema kama vile dawa.