Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshikamano wakati wa dhiki ndio faraja yangu: Midori

Mjumbe wa amani Bi. Midori nchini Mexico. Picha: UM/Video capture

Mshikamano wakati wa dhiki ndio faraja yangu: Midori

Hivi karibuni tetemeko la ardhi nchini Mexico lilisababisha vifo, majeruhi na mamia ya watu kukosa makazi. Mji wa Jojutla mkoani Morelos, ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi, na hivyo Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na serikali ya Mexico na wadau wenginewameshikamana kuwasaidia waathirika hasa kuwapa hifadhi ya muda. Mbali na mahitaji mengine ya kibinadamu, muziki ni moja ya sanaa zinazotumika kuonyesha upendo, mshikamano na pia kupitisha ujumbe wa amani unaowafanya waathirika kutojihisi wapweke.

Katika makala hii Joshua Mmali anatupeleka nchini humo ambako mjumbe wa amani Midori alishikamana na waathirika hao.