Neno la wiki: Zuzu na Bwege

15 Disemba 2017

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Zuzu" na "Bwege".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema zuzu ni mtu ambaye hana akili timamu, mtu ambaye akifunzwa hata hafunziki. Zuzu pia unaweza kumwita mjinga, zezeta au mpumbavu. Bwana Bakari akaenda mbali zaidi kuchambua neno bwege akisema halina tofauti sana na zuzu, kwa maana kwamba ni mtu nduguye. Mathalani bwege ni mtu ambaye amekaa kizoleazolea au mbumbumbu.