Magonjwa ya msimu yagharimu maisha ya zaidi ya watu 650,000

Picha ya shirika la afya ulimwenguni ikionyesha mtu mwenye magonjwa ya njia ya hewa

Magonjwa ya msimu yagharimu maisha ya zaidi ya watu 650,000

Ripoti mpya ya Shirika la afya duniani WHO na kituo cha kudhibiti wa magonjwa cha Marekani, CDC,  imesema  zaidi vifo 650,000 kila mwaka vinahusishwa na magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo homa ya mafua inayoambukiza watu nyakati tofauti za misimu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna ongezeko kubwa kutoka idadi ya vifo kati ya 250,000  na 500,000 ndani ya miaka 10 hadi kufikia zaidi ya laki sita vitokanavyo na homa  ya manjano , kisukari, magonjwa ya pumu hususani katika nchi masikini.

Dkt. Peter Salama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WHO akihusika na programu za dharura amesema idadi hiyo ni kubwa sana na ni hatarishi kwa  ukuaji wa uchumi kwani inaathiri nguvukazi katika nchi masikini, hivyo ni muhimu kuweka mikakati  ya kudhibiti majanga hayo  haraka iwezenavyo.

Aidha ripoti hiyo imeeleza kuwa waathirtika wakubwa ni watu wazima katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara,  ukanda wa mashariki ya kati na pia nchi zilizoko kusini mwa bara la Asia.

WHO  inatoa wito kwa serikali zote duniani kuwekeza katika mikakati ya kinga zaidi ili kupunguza maafa ya raia katika nchi masikini.