Seneti Mexico msipitishe muswada wa sheria Mexico: Wataalam
Muswada wa sheria mpya unaolenga kuvipatia vikosi vya ulinzi nchini Mexico kujikita na kazi za polisi bila kuwajibika kwa jamii unatia shaka kuhusu haki za binadamu
Hayo yamesemwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu hii leo huko Geneva Uswisi.
Wataalamu hao wamesema muswada huo unaotarajiwa kupitishwa leo na baraza la seneti nchini humo, unatakiwa kupingwa kwa kuzingatia hali ya kiusalama na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Mexico
Wamesema muswada huo haujatoa maelezo ya namna vikosi hivyo vitahakikisha vinazingatia haki za binadamu wakati wakitekeleza majukumu yake ambayo mengi wanaweza kuyaita ya usalama wa taifa hivyo kushindwa kuhojiwa na jamii.
Kama hiyo haitoshi, wahanga wa haki za binadamu, asasi za kiraia, mashirika ya kitaifa na kimataifa ya haki za binadamu hayajashirikishwa katika kuandaa mswada huo.
Hata hivyo wataalamu hao wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameishukuru serikali ya Mexico kwa kuonesha ushirikiano pindi walipowasiliana nao hivi karibuni kuhusu suala hilo.