Hotel iza Phuket zachukua hatua kuhifadhi baharí

14 Disemba 2017

Shirika la umoja wa matafa la mazingira UNEP limekaribisha jitihada za muungano wa hoteli za kifahari za Phuket nchini Thailand pamoja na maduka mengine makubwa kwenye ukanda huo za kujitolea katika kampeni ya  usafi wa bahari.

Anthony Lark ambaye ni mwenyekiti wa muungano huo unajumuisha hoteli za kifahari kama JW marriot, Hyatt, Hilton Novotel, swissotel na nyinginezo amesema kupitia kampeni hiyo inayoongozwa na UNEP, watasafisha fukwe ili kuepusha taka za plastiki zinazoingia baharini.

Erik Solheim ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP amesema wamepokea hatua hiyo na kukaribisha mashirika mengine kujiunga.

Zaidi ya nchini 40 zikiwemo kenya, Canada. Indonesia, Brazil na wengine  bila kusahau kampuni binafsi kama Dell na Volvo ni wanachama wa kampeni hiyo ya usafi wa bahari ya UNEP.