Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU yakanusha madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Somalia

AU Logo. Picha: AMISOM

AU yakanusha madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Somalia

Tume ya muungano wa Afrika imekanusha madai ya ukiukaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na vikosi vyake vya kulinda amani nchini Somalia AMISOM, madai yaliyopo katika ripoti ya pamoja iliyozinduliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na na kundi la ulinzi wa raia HRPG.

Tume hiyo ya AU inasema imetambua kwa masikitiko mdai ya ripoti hiyo ya “Ulinzi wa raia:ujenzi wa msingi wa amani, usalama na haki za binadamu” iliyotolewa mwishoni mwa juma, ambayo inasema imewasilisha visivyo baadhi ya matukio yanayohusu operesheni za AMISOM za ulinzi wa raia nchini Somalia.

Tume hiyo ya AU inasema  ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ilipuuza matokeo ya uchunguzi uliofanywa na idara maalumu ya upelelezi ya AMISOM na hii ni licha ya AMISOM kutoa ulinzi wa kwachunguzi wa Umoja wa Mataifa kuendesha uchunguzi wao huru.

AU inataka kueleza kwamba vikosi vya AMISOM havikukutwa na hatia katika matukio ya tarehe 7 Mei 2016 na tukio la Bulo-Butro la April 2016 yaliyoorodheshwa kwenye ripoti ya Umoja wa Mataifa  yakihusiana na visa vya ubakaji unaodaiwa kufanywa na wanajeshi wa AMISOM , baada ya tume ya uchunguzi kushindwa kuwasilisha ushahidi wowote kwamba vikosi hivyo vilitekeleza vitendo hivyo ambavyo ni kukiuka haki za binadamu.

Kwa mujibu wa AU ripoti hiyo ambayo inawashutumu pia wanajeshi wa AMISOM kwa ukatili na mauaji ya raia 178 katika kipindi cha Januari 2016 hadi 14 Oktoba 2017 imeshindwa kutoa ushahidi wa kuunga mkono madai hayo na inasema pia imeshindwa kutilia maanani moyo ambayo umejengeka wa ushirika baiana ya AMISOM na ofisi ya UNSOM ya sera za kudumisha haki za binadamu nchini humo (HRDDP)