Ukimpa mwanamke fursa, jamii itanufaika

12 Disemba 2017

Kuna usemi wa kwamba ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii na ukielimisha  jamii basi utakua umeokoa  kizazi cha baadaye. Huu usemi  hauna maana ya upendeleo bali  ni ukweli kwamba ukimpa mwanamke fursa basi  jamii itanufaika zaidi. Hii inatokana na mapenzi, malezi, na moyo wa ujasiri aliojaliwa  mwanamke.

Kwamaniki hiyo tunao mfano ya Bi Magdalena Namutebi mwanamke shupavu na shujaa, ambaye mbali na matatizo ya kufiwa na mume wake  miongo mitatu iliyopita, peke yake alifanikwa kulea familia  yenye zaidi ya  watoto 9, kwa kuwapata fursa ya elimu na malezi bora. Tuungane na mwandishi weu John Kibego kutoka Uganda katika Makala hii.