Djibouti yafuata nyayo kuwakumbatia wakimbizi, UNHCR yakaribisha

12 Disemba 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekaribisha  kwa furaha sheria mpya iliyopitishwa nchini Djibouti inayowapatia wakimbizi walioko nchini humo fursa ya  kupata huduma za msingi za kijamii bila vikwazo. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Kwa mujibu wa UNHCR, sheria hiyo mpya inayowapa wakimbizi nafasi ya kupata elimukuingia katika soko la ajira, kushiriki masuala ya kiuchumi na piahuduma za afya imepitishwa  tarehe 7 Desember chini ya uongozi wa rais Omar Guelleh na pia ni sehemu ya makubaliano kati ya serikali ya Djibouti na UNHCR yaliyoafikiwa mwezi Agosti mwaka huu  yakihimiza nchi zinazohifadhi wakimbizi kuhakikisha zinatoa elimu bora kwa watoto wote wakimbizi kwa kuwahusisha katika mfumo wa kitaifa.

Akifafanua Zaidi hatua hiyo ya serikali ya Djibouti msemaji wa UNHCR Adrian Edward amesema wakimbizi wanastahili kupata huduma zote za msingi kule wanakohifadhiwa na mara nyingi wakishirikishwa wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi zinazowahifadhi na hivyo

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

“Ijulikane tu kwamba upitishwaji wa sheria hii mpya  chini Djibuti ni mwendelezo wa ahadi za Rais Omar Guelleh alizozitoa katika mkutano wa ngazi ya juu ya viongozi mwaka jana, baada ya kupitishwa kwa zzimio la New York la wakimbizi na wahamiaji mwezi Septemba 2016.”

Djibouti  ambayo ni moja ya nchi inayohifadhi wakimbizi zaidi ya 27,000, pia ni mweyenji wa  mkutano wa kikanda wiki hii unaojadili kuhusu uboreshaji wa elimu kwa wakimbizi kwa kuzingatia mfumo wa  kimataifa wa kutetea haki za wakimbizi .

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter