Utunzaji misitu ni jawabu la mabadiliko ya tabianchi
Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaziasa serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia duniani kote kuongeza jitihada katika zoezi la kulinda mazingira.
Upandaji miti na uhifadhi wa misitu miti ni moja ya hatua muhimu sana katika kukabiliana na tatizo la ukame katika nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara.
Nchini Uganda kampeni ya upandaji miti na uhifadhi wa misitu inaendelea vizuri kufuatia hatua ya serikali kuweka mkazo swala la ulinzi wa misitu. Mwandishi wetu John kibego alipata fursa ya kuwatembelea wananchi wa Rwangara nchini Uganda, ambao wamekuwa wakihifadhi misitu kwa manufaa ya kulinda mazingira.