Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfiwa huambiwa Makiwa na si pole- Sigalla

Neno la wiki_MAKIWA

Mfiwa huambiwa Makiwa na si pole- Sigalla

Wiki hii tunaangazia neno “Makiwa” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno Makiwa ni salamu ya heshima na unyenyekevu inayotolewa kwenye nyumba ya wafiwa. Mtu akiambia Makiwa, mfiwa anajibu "Tunayo" kama marehemu hajazikwa au "Yamepita" kama tayari marehemu amezikwa. Hata hivyo mazoea ni neno "Pole" ambalo mchambuzi anasema halifai sana.