Amani na haki ndio msingi wa kundi letu:Dance for Peace

8 Disemba 2017

Amani , haki sawa kwa wote na taasisi imara ndio kauli mbiu ya kundi la Dance for Peace au cheza kwa ajili ya amani linalojihusisha na muziki wa oprea na unenguaji. Kundi hili mashuhuri hapa Marekani linalojumuisha wanawake wa nchi hii limekuwa likifanya mataonyesho mbalimbali kuielimisha jamii kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG's na hususani lengo namba 16 linalohimiza amani, haki sawa kwa wote na taasisi imara. Leo limekuja hapa kwenye  makau makuu ya Umoja wa mataifa Newyork  katika kampeni ya kuchagia haki na amani duniani, iwakitumia talanta zao za kuimba na kunengua kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa amani na haki. Shuhuda wetu kwenye onyesho hilo ni Patrick Newman ambaye ameandaa makala hii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud