Walinda amani 12 wauawa DRC, UM wagubikwa na majonzi

8 Disemba 2017

Walinda amani 12 kutoka Tanzania wameuawa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Nats..

Sauti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitangaza kwa majonzi kuuawa kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC jimbo la Kivu Kusini.

(Sauti ya Antonio Guterres)

“dalili za awali kwenye eneo la tukio Kivu ya Kaskazini zinaonyesha kwamba takribani walinda amani 12 wa Tanzania wameuawa , wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa na wanne kati yao wako hali mahtuti na tunaelewa kwamba wanajeshi watano wa jeshi la serikali ya DRC nao wameuawa.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwenye mkutano wa kuchangia mfuko wa dharura wa UM (CERF) ambako ndipo alipoanza hotuba yake kwa kuzungumzia mashambulizi dhidi ya walinda amani wa umoja huo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. (Picha:UN/Rick Bajornas)

Yaelezwa kuwa walinda amani hao walio kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO walikabiliwa na mashambulizi kutoka kikundi cha waasi cha ADF.(Sauti ya Antonio Guterres)

“Hili ni shambulio baya zaidi kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika historia ya karibuni, nalaani shambulio hili kwa kila hali, na mashambulio haya dhidi ya walinda amani wa Umoja hayakubaliki na ynaweza kuwa uhalifu wa kivita.”

Ametuma rambirambi kwa serikali ya Tanzania na familia za waliouawa na kuwatakia majeruhi ahueni ya haraka akiongeza kwamba mashambulio kama haya yanadhihirisha umuhimu wa kumaliza migogoro na kudumisha amani.

Mara baada ya Katibu mkuu kuzungumza Flora Nducha wa Idhaa hii alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga ambaye amesema..

(sauti  ya balozi Augustine Mahiga)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter