Uganda yadhibiti mlipuko wa homa ya Marburg

8 Disemba 2017

Shirika la Afya Duniani  WHO, limesema, Uganda imefanikiwa kudhibiti mlipuko wa homa ya marburg wiki chache tu baada ya ugonjwa huo kuzuka.

Mkurungezi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti  amesema mara baada ya kuripotiwa kwa ugonhwa huo tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka huu, kwenye maeneo ya mpakani, serikali ya Uganda ilichukua hatua.

Mathalani walianzisha kwa kushirikiana na WHO, walianzisha ofisi ya huduma ya  dharura ya afya kwa uuma katika wilaya ya Kween na Kapchorwa mashariki mwa Uganda, mpakani na Kenya, ili kukabiliana na mlipuko huo.

Ugonjwa huo ulisababisha vifo vya watu watatu na wengine 360 waliosadikiwa kuwa karibu na waliofariki dunia waliwekwa chini ya uangalizi wa kitabibu.

Dkt Moeti, amesema Uganda imekuwa mfano wakuigwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na  mamlaka za afya na washirika wake kwa kuwa kwa msaada wa WHO waliweza kuchunguza na kudhibiti kuenea kwa virusi vya homa ya Marburg ndani ya wiki kadhaa tu.

Naye Sarah Opendi ambaye ni waziri wa afya Uganda amesema wizara yake ilitanganza kudhibiti ugonjwa huo baada ya kujiridhisha na kutokuwepo kwa kisa kingine cha mgonjwa siku 21 baada ya kisa cha mwisho katika maeneo yaliyokuwa yameathiriwa.

WHO imesema inaendelea kusaidia mamlaka ya afya katika nchi zote mbili ili kuboresha uwezo wao wa ufuatiliaji majibu, ikiwa ni pamoja na hatua za kuzuia na kudhibiti, na usimamizi .

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter