Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la haki latulinda sote, hivyo tulitetee- Guterres

Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa. Picha: UM

Azimio la haki latulinda sote, hivyo tulitetee- Guterres

Kwa pamoja tusimame na tuzungumze kuhusu haki za binadamu kwani zinatulinda sote! Hiyo ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani tarehe 10 mwezi huu siku ya jumapili.

Siku hii inaadhimishwa kukumbuka kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu la duniani tarehe 10 disemba mwaka 1948 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, azimio ambapo Bwana Guterres amesema linaweka misingi ya usawa na utu kwa kila mtu.

Amesema azimio hilo limefanya serikali ziwajibike katika kuhakikisha zinalinda haki za msingi na uhuru wa watu.

Ingawa hivyo amesema hii leo ulimwenguni unashuhudia ukatili dhidi ya binadamu katika kila kanda hivyo..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Kwa pamoja tusimame kupinga mienendo hii mibaya. Azimio la haki za binadamu ndio nyaraka iliyotafsiriwa zaidi duniani.Kwa pamoja tuhakikishe maneno yanatafsiriwa kwa vitendo.”

Wakati huo huo, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein  amesema azimio hilo lililotafsiriwa kwa lugha nyingi zaidi duniani limesaidia kuboresha maisha ya mamilioni ya watu ulimwenguni.

Hata hivyo amesema bado kuna madhila duniani ikiwemo viongozi wa kisiasa kupingana na Ibara ya kwanza ya azimio hilo isemalo kila binadamu amezaliwa huru na sawa kwa utu na haki.

Kwa mantiki hiyo amesema maadhimisho ya miaka 70 ya azimio hilo yanapoanza, ni vyema kuheshimu waasisi wa azimio hilo huku kila mtu akihaha kulinda misingi yake.

Awali akizungumza na Idhaa hii kuhusu utekelezaji wa tamko hilo, Mutuma Ruteere, ambaye ni mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa mstaafu amesema..

(sauti ya Mutuma Ruteere)