Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina hisia za kushindwa katika suala la Syria: Egeland

Jan Egeland akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Uswisi. (Picha: UN/Luca Solari)

Nina hisia za kushindwa katika suala la Syria: Egeland

Ukosefu wa kufikishwa misaada kwa jamii nyingi zinazoihitaji zaidi Syria na kura ya turufu inayoendelea kuwa kikwazo cha kuwahamisha mamia ya wagonjwa walio katika hali mbaya ni hisia kama ya "kushindwa", amesema leo mshauri mwandamizi wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis ,Jan Egeland ameeleza kwamba katika eneo linalodhibitiwa na wapinzani la Mashariki mwa Ghouta nje yam ji mkuu Damascus, wiki nyingine imekatika bila fursa ya misafara ya misaada kuingia.

Karibu watu 500 bado wanahitaji msaada wa haraka wa matibabu na hii ni hali mbaya ya kusikitisha akiongeza kuwa

(SAUTI YA JAN EGELAND)

“Sisi kama watoa huduma za kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa na pia mashirika yasiyo ya kiserikali tunahisia Kali zakuchanganyikiwa na hasira, kwa sababu tumejiandaa, tuko tayari na tunaweza kuokoa maisha , kuwahamisha majeruhi na wagonjwa kutoka eneo linalozingirwa la Mashariki mwa Ghouta, kutoa msaada kwa watoto wenye utapia mlo katika eneo hilo lakini tunazuliwa, tunakataliwa kwa sababu za kisiasa na kiusalama na pande zilizopo hapo, na serikali ya Syria na hatusaidiwi kama tunavyopaswa na nchi ambazo zina ushawishi  na hali hiyo, hivyo nina hisia za kushindwa kwa kweli.”