Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni changamoto kupata dawa za kupambana na ukimwi Africa magharibi na kati: UNICEF/UNAIDS

Watoto wanne kati ya watano wanaoishi na VVU Afrika Magharibi na Kati bado hawapokei tiba ya kupambana na virusi vya ukimwi. Picha: UNICEF

Ni changamoto kupata dawa za kupambana na ukimwi Africa magharibi na kati: UNICEF/UNAIDS

Ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa matraifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la kupambana na ukimwi UNAIDS inasema  watoto wanne kati ya watano wanaoishi na virusi vya ukimwi au VVU Afrika Magharibi na Kati hawapati dawa za kupunguza makali ya ukimwi,  huku vifo vinavyohusiana na ukimwi miongoni mwa  vijana barubaru wa umri wa miaka 15-19 vikiongezeka. Selina Jerobon na taarifa kamili.

(TAARIFA YA SELINA)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wakati kuna mafanikio katika baadhi ya sehemu duniani katika vita dhidi ya ukimwi ,  mwaka 2016 zaidi ya watoto 60,000 wameambukizwa VVU ukanda wa Afrika Magaribi na kati.

Bwana Marie-Pierre Poirie ambaye ni mkurungezi wa UNICEF Afrika Magharibi  na Kati amsema  kuna umuhimu wa kutumia fursa mpya ya vifa vya kisasa kubaini ugonjwa huo mapema ili kuweza kuwaanzishia waathirika  taratibu za mataibabu mapema, jambo ambalo litaokoa maisha ya watoto na vijana wengi .

Aidha amesema kutokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu husuni vijana katika nchi kama Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo  DRC na Nigeria, vifo vya vijana ambao ni waathirika wa VVU vitaendelea kua juu, hivyo lazima serikali na taasisi za afya zizingatie uelimiswaji wa jaami kuhusu ugonjwa wa ukimwi.

Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba watoto wengi na barubaru wanapoteza Maisha kwa sababu tu hawajapimwa na kupokea matibabu yanayostahiki. Amezisihi serikali za nchi husika kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma linapokuja suala la ukimwi.