Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna haja ya kuboresha kiwango cha hewa ya ukaa kwenye udongo:FAO

Mwanamke apnda mbegu shambani mwake. Picha: FAO

Kuna haja ya kuboresha kiwango cha hewa ya ukaa kwenye udongo:FAO

Katika kuadhimisha siku ya udongo duniani hii leo  Desemba 5, shirika la chakula na kilimo duniani FAO limezindua ramani ya kina ya dunia inayoonyesha kiwango cha hewa ukaa kwenye udogo.

Shirika hilo linasema mchanganyiko wa chembechembe asili na hewa ukaa ni muhimu sana kwa rutuba ya udogo na uwezo wake wa kuzalisha, kupenyeza maji na kuyahifadhi, lakini pia katika uzalishaji wa chakula.

Na kama muhifadhi mkuu wa hewa ya ukaa, kuutunza na kurejesha udongo katika rutuba ni suala la kupewa kipaumbele kwa ajili ya kilimo endelevu na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ramani hiyo inaonyesha kimataifa asilimia 30 za kwanza za udongo zina takriban tani bilioni 680 za hewa ukaa karibu mara mbili ya hewa ukaa iliyo hewani na FAO inasema hicho ni kiwango kikubwa kuliko hewa ukaa yote inayohifadhiwa katika mimea ambayo ni tani bilioni 560, na asilimia 60 ya hewa ukaa hiyo inapatikana katika nchi kumi zikiwemo Marekani, Urusi, Canada, uchina , Brazili na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Ronald Vargas ni afisa wa masuala ya ardhi na maji wa FAO

(RONALD CUT)

“Udogo ndio wenye jukumu la kuzalisha mazao, siku hizi watu wanajaribu kuzalisha zaidi katika ardhi ndogo, hivyo matumizi ya kupindukia ya kemikali sio njia sahihi kwa sababu  yanaweza kuwa na athari mbaya kwenye rutuba ya udogo na hiyo inaweza kuleta zahma sio tuu kwa uhakika wa chakula bali pia katika malengo yote ya SDG’s”