Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutapata habari za kina kuhusu Yemen Kesho: UM

Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Salehe kulia). Picha: UM/Mark Garten

Tutapata habari za kina kuhusu Yemen Kesho: UM

Umoja wa Mataifa umesema unasubiri taarifa za mjumbe wake maalum kwa Yemen kuhusu taarifa zinazodai kuuawa kwa rais wa zamani wa nchi  hiyo Ali Abdullah Salehe.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema hawana taarifa za kina kuhusu habari hizo na kwamba..

(Sauti ya Dujarric)

‘‘Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed yupo Riyadh akikutana na maaafisa wa Saudi Arabia na anatarajiwa kurejea kesho ambapo atalihutbia Baraza la Usalama katika mkutano wa wazi kwa njia ya video. Natumaini atakuwa na mengi ya kusema kuhusu athari za kisiasa za kile kinachotokea.’’

Akizungumzia hali ya sasa ya Yemen na kinachondelea, Bwana Dujarric amesema..

(Sauti Dujarric)

‘‘Kawaida inaongeza kiwango kikubwa cha madhila kwa hali mbaya sana ya kisiasa. Tumeshuhudia kuibuka kwa machafuko kunakoogofya mjini Sana'a katika siku chache zilizopita. Hili linaongeza mateso mengine kwa watu hususani walioko  mjni Sanaa ambako miundombuni inalengwa.’’