WHO yatoa msaada wa vifaa vya tiba Libya
Shirika la afya duniani WHO limetoa msaada wa mitambo ya kusaidia kupumua kwa wangonjwa mahututi katika hospitali ya Tragen kusini mwa Libya
Msaada huo wa mitambo miwili pamoja na vipuri vyake vyote umetolewa kufuatia kuwepo na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo vya tiba kwa wagonjwa mahututi na wenye kuhitaji usaidizi wa kupumua.
WHO imeeleza kujizatiti kuendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwenye nyanja ya afya maeneo yote nchini Libya .
Fedha za kununulia vifaa tiba hivyo zimetoka kwenye mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF