Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji zaidi wahitajika ili kukabiliana na njaa- FAO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva. Picha: FAO

Uwekezaji zaidi wahitajika ili kukabiliana na njaa- FAO

Ongezeko la idadi ya watu wenye njaa duniani ni kiashiria kuwa mbinu mpya zahijitaka ili kubadili mwelekeo huo.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema hayo akihutubia kikao cha baraza la shirika hilo mjini  Roma, Italia.

Amenukuu takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa idadi ya watu wenye njaa ni milioni 815, ikiwa ni ongezeko la kwanza katika kipindi cha zaid ya muongo mmoja.

Bwana da Silva amesema njaa inakwenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu wenye utipwatipwa  katika nchi maskini na tajiri na hivyo kuweka changamoto nyingine katika mfumo wa sasa wa chakula.

Kwa mantiki hiyo Mkurugenzi Mkuu huyo wa FAO amesema jambo la msingi ni kujenga uwezo wa watu maskini hususan kwenye mizozo kuweza kukabiliana na njaa, ambapo mifumo ya usaidizi wa kibinadamu  iende sambamba na misaada ya kuwawezesha kujipatia kipato.

Amesema hatua hiyo inamaanisha uwekezaji mpya kutoka sekta binafsi na ya umma ili kuinua fursa za kujikimu za wananchi katika sekta mbali mbali ikiwemo kilimo na ufugaji.