Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasaka hifadhi na wakimbizi vijana waona nuru huko Ujerumani

Picha na UM
Muziki umekuwa njia nzuri kwa wakimbizi nchini Ujerumani kuboresha lugha ya Kijerumani. Picha: UNHCR

Wasaka hifadhi na wakimbizi vijana waona nuru huko Ujerumani

Stahamala na utangamano ni mambo ambayo Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ikiwemo lile la wakimbizi duniani, UNHCR unapigia chepuo kila uchao. Hatua hiyo inatatokana na ukweli kwamba mambo hayo mawili ni muhimu wakati huu ambapo idadi ya watu wanaosaka hifadhi ugenini inaongezeka kila uchao. Stahamala huwezesha watu wa rangi,  jinsia au utaifa tofauti kuishi pamoja na hivyo kuimarisha ustawi wao. Na hivyo ndiyo inavyofanyika huko Ujerumani, nchi ambayo inapokea wakimbizi na wahamiaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anakupeleka mjini Berlin.