Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita, majanga vyaongeza mahitaji ya usaidizi wa kibinadamu

Pichani ni eneo le Jeremie nchini Haiti ambako baada ya kimbunga Matthew kilichopiga Haiti mwaka jana watu zaidi ya 750,000 walihitaji misaada ya dharura ya kibinadamu. (Picha:IOM/Hajer Naili)

Vita, majanga vyaongeza mahitaji ya usaidizi wa kibinadamu

Kiasi cha dola Bilioni 22 nukta 5 kinahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2018 unaolenga kuwafikia watu milioni 91.

Ombi hilo la fedha limeongezeka kutoka bilioni 22 nukta 2 mwaka jana kutokana na vita, majanga ya asili, milipuko ya magonjwa na kutafuta makazi kusababisha ongezeko la mahitaji ya usaidizi wa kibinaadamu.

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock akiwa Geneva, Uswisi ametangaza ombi hilo leo huko Geneva, Uswisi huku akiomba wahisani zaidi kujitolea kuchangia.

(Sauti ya Mark Lowcock)

“Ambako tunatoa msaada bora, tunaokoa maisha. Lakini pia tunalinda mustakhbali mkubwa. Inatugharimu takribani sentí 77 kwa siku ili kutoa usaidizi wa kina tuliopanga kupitia ombi hili. Huo ni uwekezaji rahisi zaidi unaoweza kufanya kwa ajili ya usalama wa binadamu an utu. Kwa hiyo tunatumaini kuwa kwa msingi wa ubora wa mipango yetu tutaweza kufikia kiwango cha juu cha ufadhili kuliko vile tumesema tumefikia mwaka huu.”

Hali ya kibinadamu inatia shaka ambako nchini Yemen, mtoto mmoja anafariki dunia kila baada ya dakika 10, ambapo Bwana Lowcock amesema nchi hiyo inaweza kusalia kuwa yenye janga baya zaidi duniani.

image
Hapa ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wanawake wakishiriki katika programu ya kazi ili kupata fedha za kujikimu kupitia mradi wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM.Ni baada ya vita kusambaratisha njia zao za kujipatia kipato. (Picha: IOM/Amanda Nero )