Skip to main content

Wakati maelfu ya Wacongo wakikimbilia Zambia, fedha za misaada zakauka:UNHCR

Wakimbizi wa DRC waelekea nchi zinginekufuatia vurugu. Picha: UNHCR

Wakati maelfu ya Wacongo wakikimbilia Zambia, fedha za misaada zakauka:UNHCR

Idadi ya watu wanaokimbia machafuko ya wanamgambo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na kuingia Zambia sasa imepita 12,000, huku watu zaidi ya 8400 wakiwasili katika miezi mitatu iliyopita.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo, ikiongeza kuwa asilimia 80 ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto wanaokimbia ukatili wa hali ya juu unaotekelezwa na wanamgambo ikiwemo mauaji ya raia ubakaji wa wanawake, uporaji wa mali binafasi na nyumba kuchomwa moto.

Wengi wa wakimbizi hao wanatoka katika majimbo ya Haut-Katanga na Tanganyika na kuingia kwenye jimbo la Luapula Zambia ambako wanapewa hifadhi kwenye kambi ya muda ya Kenani Nchelenge .UNHCR inasema kambi hiyo imefurika hivi sasa ikihifadhi watu zaidi ya 8000 na kukabiliwa na tatizo kubwa la fedha kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR Babar Baloch

(BARBAR BALOCH CUT)

Shughuli za kibinadamu DRC na Zambia zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili, dola milioni 236.2 zinahitajika ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wengineo . Nchini DRC ni dola milioni 54.6 tu ndizo zilizopokelewa hadi sasa  na Zambia dola milioni 13.6 tu zimepatikana. Katika visa vyote hivi fedha zillizopatikana ni chini ya robo ya fedha zinazohitajika”

Zambia hivi sasa inahifadhi jumla ya wakimbizi 65,000 wakiwemo wakimbizi 33,000 kutoka DRC.