Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila huduma dhidi ya VVU ningalikuwa mfu hivi sasa- Mpho

Mpho Tlabaki, mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa wanaume kukubali kupima virusi vya ukimwi, VVU. Picha: UNAIDS/Video capture

Bila huduma dhidi ya VVU ningalikuwa mfu hivi sasa- Mpho

Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi duniani, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kuwa wanaume ni wagumu zaidi kukubali kupima Virusi Vya Ukimwi, kuliko wanawake. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora Nducha)

Huyu ni Mpho Tlabaki mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa wanaume kukubali kupima virusi vya ukimwi, VVU.

(Sauti ya Mpho Tlabaki)

“Niligundua kuwa wanaume wanakosa uelewa kuhusu afya kwasababu kwa upande wangu nilipima mara mbili nikakutwa nina VVU lakini sikuamini. Kwa ujumla wanaume hawana uelewa na wengi wao wanasaka ushauri kwa waganga wa kienyeji badala ya kwenda hospitali.”

UNAIDS inasema pamoja na kukosa uelewa, wanaume pia ni wagumu kufuatilia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi na pia wako hatarini zaidi kufariki dunia kutokana na Ukimwi kuliko wanawake.

image
Harakati za kupima VVUs. Picha: UNAIDS/Video capture
Katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, wanawake na wasichana wako tayari mara 60 zaidi kufahamu hali yao kuhusu Ukimwi kuliko wanaume na wavulana.

Tayari serikali ya Lesotho imewezesha uwepo wa wauguzi wanaofuata wagonjwa majumbani ikiwemo Mpho ili kufuatilia matumizi ya dawa.

(Sauti ya Mpho Tlabaki)

 “Matibabu yamebadili maisha yangu. Bila matibabu ningalikuwa mfu hivi sasa kwa sababu matibabu yamenipatia nguvu na sasa nimerejea kazini. Niseme tu yameniwezesha kuishi na kujisikia tena nina nguvu.”

Nchini Burundi matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi yameongezeka kutoka watu 10,000 mwaka 2007 hadi watu 52,000 mwaka huu wa 2017.

Hata hivyo Vena Hamza Burikukiye anayeishi na VVU ni kiongozi wa shirika la kutetea watu wenye Ukimwi CAPESPlus anasema..

(Sauti ya Vena Hamza Burikukiye)