Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamthilia ya kuhimiza maelewano baada ya mifarakano Uganda yashinda tuzo UNAOC

Jane Ajuang kutoka shirika la Media Focus on Africa Uganda aanapokea tuzo ya muingiliano wa kiutamaduni duniani, UNAOC. Picha: UM/Leah Mushi

Tamthilia ya kuhimiza maelewano baada ya mifarakano Uganda yashinda tuzo UNAOC

Jane Ajuang kutoka shirika la kiraia la Media Focus on Africa nchini Uganda ameshinda tuzo ya mwaka huu ya muingiliano wa kiutamaduni duniani.

Jane amekabidhiwa tuzo hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani , tuzo ambayo hutolewa kwa ushirikiano kati ya Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa UNAOC na kampuni ya BMW.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa baada ya kupokea tuzo hiyo, Jane amesema ushindi wake umetokana na yeyé kubuni tamthilia iliyowezesha makabila yaliyopigana vita nchini Uganda kuungana pamoja na kushirikiana.

(Sauti ya Jane Ajwang)

Jumla ya maombi 1356 yenye miradi mbalimbali bunifu katika kuleta maelewano yaliwasilishwa kutoka nchi 130 ambapo miradi 10 iliingia kwenye kinyang’anyiro cha mwisho.

image
Washindi wa tuzo ya matumizi ya mbinu bunifu katika kujenga maelewano ya kiutamaduni: (Picha:UNAOC)