Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Palestina na Israeli wakae meza moja kumaliza tofauti zao : Guterres

Meza kuu katika kikao mahsusi cha kuadhimisha siku ya mshikamano na watu wa Palestina. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwakilishwa na Naibu wake Amina J. Mohammed, (wa pili kutoka kushoto) Picha: (UN/Kim Haughton)

Palestina na Israeli wakae meza moja kumaliza tofauti zao : Guterres

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na wapalestina, ili kujadili mustakabali wa eneo hilo ambalo limekuwa katika migogoro kwa miongo zaidi ya mitano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia naibu wake, Amina J. Mohammed, amerejelea wito wake kwa waisreli na wapalestina kukaa meza moja na kutafuta suhulu ya mgogoro uliodumu kwa kipindi kiferu sasa.

Bi. Amina amesema suluhu ya mataifa mawili kati ya  Israeli na Palestina ni miongoni ya masuala ambayo Umoja wa mataifa haujapatia ufumbuzi, hivyo maendeleo ya wapalestina yanaathirika zaidi kuliko kwa Israeli.

image
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akihutubia kikao cha Baraza Kuu wakati wa siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. (Picha:UN /Kim Haughton)
 (Sauti ya Bi. Amina J. Mohammed)

 “Miaka 70 iliyopita tangu kupitishwa kwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 181 ambalo ni suluhu ya mataifa mawili,  bado hatujafikia hatua ya  kuwa na taifa huru la wapalestina sambamba na taifa la Israel. Ila bado naamini kwamba utekelezaji wa azimio hilo la uwepo wa mataifa mawili kati ya wapalestina na waisraeli unawezekana endapo pande zote zitakaa meza moja na kutafuta suluhu itakayosababisha amani na utulivu katika ukanda wa Mashariki ya Kati.